Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake.Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.
Ommy na Vanessa Mdee.“Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa,”ameandika Ommy.“Ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane……Asante @vanessamdee kwa kupokea na fuko langu.”