Monday, October 20, 2014

DR. CHENI: RUSHWA YA NGONO WANAITAKA WENYEWE, HAKUNA ANAYEWALAZIMISHA


Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na kudai wanaziendekeza wao wenyewe.

Akiongea na mwandishi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia zinavyowasukuma.
 
“Sizani kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu ya watu wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo nakubali sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana, sidhani kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu, mpaka watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana,” alisema Dk. Cheni.