Monday, October 20, 2014

IMEKAA POA SANA! MENEJA WA WEMA, MARTIN KADINDA AMFUATA JACK PATRICK GEREZANI! SHUKA NAYO HAPA!

Imekaa poa sana! Ubuyu kutoka Hong Kong, China unadai kwamba mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda hivi karibuni alimfuata Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani aliyefungwa nchini humo kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya.
 
Martin Kadinda wakati  akiwa na Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
 Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Isaac Sepetu zilidai kwamba katika safari yake nchini humo, alifuatana na Wema na Petit Man.
Mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda akipozi.
 “Kadinda amepongezwa sana kwa hatua yake hiyo, kuhusu kama alionana naye au alichoongea naye, tusubiri arudi maana bado yupo China,” alisema rafiki wa mmiliki huyo wa lebo za mavazi za Single Button na Kwachukwachu.