Wednesday, October 15, 2014

FACEBOOK KUWALIPA WAFANYAKAZI WAKE WA KIKE KUGANDISHA MAYAI YA UZAZI ILI WASIZAE NA WAFANYE KAZI KWA BIDII ZAIDI!

Makampuni ya Facebook na Apple yanawapa nafasi wafanyakazi wake wa kike kuweka pembeni ndoto zao za kuwa mama kwa kuwalipa wagandishe mayai yao. 



Hatua hiyo isiyo ya kawaida ina lengo la kuongeza idadi ya wafanyakazi wa kike kwa kuwaruhusu kujikita zaidi na masuala ya kazi bila kupoteza ndoto zao kwa kuwa na watoto baadaye katika maisha yao. 


Bank: Mayai yatakuwa yakiweka kwenye freezer maalum ili wanawake waendelee na kazi zao

Makampuni hayo ya Silicon Valley ni ya kwanza kutoa ofa hiyo bila sababu za kitabibu na yako tayari £12,500 kwa kila mmoja kugharamia mchakato huo. 

Kwa mujibu a NBC News, Facebook imeshaanza kulipia mchakato huo na Apple wataanza January.

-via:udakumagazine