Wednesday, October 22, 2014

HIZI NDIO PICHA 11 KUTOKA KEKO, NYUMBANI KWENYE MSIBA WA MSANII YP.

YP IIIAliyekuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, YP ambaye amefariki usiku wa jana katika hospitali ya Temeke wakati alipokuwa akitibiwa maradhi ya kifua kikuu (TB) anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho katika makaburi ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, YP ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambilikile ameugua kwa kipindi cha takribani miezi 2 kabla ya kufikwa na umauti hapo jana.
Hizi ni picha 11 za kutoka eneo la Keko, nyumbani alikokuwa akiishi msanii marehemu ambapo taratibu za mazishi zinafanyika.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.