Saturday, October 18, 2014

JAMBO LIMEZUA JAMBO.. RAYUU AMTAKA WOLPER AKAPIME UKIMWI

MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye.
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema anamheshimu Wolper na kamwe hawezi kumsema vibaya lakini alishangaa kuambiwa na mashosti wake kwamba anamsema yeye ana Ukimwi.
“Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
“Kutokana na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu yake.”
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Kutokana na mtafaruku huo, mapaparazi wetu walifanya juhudi za kumsaka Wolper pasipo kuzaa matunda, ambapo simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wenye mlolongo mzima wa ishu hiyo, hakujibu.