Saturday, October 18, 2014

ILE MELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI YAZUIWA MEXICO KISA YAHOFIWA KUWA NA WAGONJWA WA EBOLA

Meli ya Carnival Magic ya Marekani (Picha na Maktaba).
Meli ya Carnival Magic ya Marekani imezuiwa kutia nanga katika kisiwa cha Mexico cha Cozumel ikihofiwa kuwa na mgonjwa wa Ebola.
Meli hiyo iliondoka katika jimbo la Texas ikiwa na mhudumu mmoja wa afya ambaye alikuwa amehudumia sampuli za mgonjwa wa ebola marehemu Thomas Duncan aliyeaga dunia kutokana na ugonjwa huo.
Afisa mmoja katika bandari ya Mexico alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa we ebola.
Mhudumu huyo wa afya ambaye amejitenga pamoja na mumewe wakiwa kwenye meli hiyo yuko chini ya uangalizi kwa ameonyesha dalili za ugonjwa huo.