Wednesday, October 8, 2014

MAMA WEMA ATAKA MAHARI YA MIL.100 ILI DIAMOND AMUOE MWANAE....WEMA SEPETU ASEMA YUPO TAYARI KUOLEWA HATA BURE NA DIAMOND


Habari ya mjini hivi  sasa  ni  Ndoa ya  msataa wa Bongo, Wema  Sepetu  na  Diamond Platnumz.
 
Habari  zinaarifu kuwa ili Diamond Platnumz  aweze kumuoa Wema Sepetu ni lazima atoe shilingi milioni mil. 100.
 
Habari  hizi  ni  kwa  mujibu wa gazeti moja la udaku  lililotoka Jana  ambapo  liliripoti kuwa mama Wema sepetu anataka mahari ya milioni 90 na ushee ili binti yake huyo asiyechuja umaarufu awe mkwe wa mama Diamond.
 
Inadaiwa kuwa sherehe za birthday za Wema na Diamond zilizofanyika hivi karibuni na kugharimu pesa nyingi ndiyo zinadaiwa kumtia hamasa  mama Wema na kutaka mahari hiyo kubwa kwa madai kuwa Diamond anazo pesa  na hashindwi kutoa pesa hiyo ili kumuoa Wema ambaye umaarufu wao wote wawili ni mkubwa sana hapa Tanzaia huku umaarufu wa Diamond nje ya Tanzania ukiwa mkubwa zaidi  kuliko wa Wema.

Hata hivyo habari zaidi zinadai kuwa Wema mwenyewe yupo tayari kuolewa hata bure na Diamond.