Wednesday, October 8, 2014

MILIONI 30 ZA JOHARI ZIMEPOTEA BAADA YA KUZUILIWA KUTOKA KWA FILAMU YA SISTER MARRY


Muigizaji wa filamu Blandina Chagula aka Johari amesema pamoja na kusikitishwa kutokana na bodi ya filamu nchini kuizua filamu ya ‘Sister Marry’ isitoke, amekula hasara kubwa.

Johari amesema  kuwa maandalizi ya filamu hiyo yalighalimu shilingi milioni 30.
 
“Unajua inauma sana, tumeshindwa kutetea filamu ya ‘Sister Marry’ kutokana na madai eti tumedhalilisha dini. Ina maana hawataki tuzungumzie maisha halisi kwenye filamu zetu? 
 
"Mimi binafsi imeniumiza sana. Ile filamu imegharimu zaidi ya milioni 30, hebu angalia, Halafu inafungiwa ili isitoke kabisa!
 
"Kinachonisikitisha ni kwamba serikali yetu inashindwa kuangalia sisi tunavumbua baadhi ya maovu ya watu ambayo wanayafanya ili kuelimisha jamii.
 
"Kwahiyo imefungiwa na kukatazwa isitoke kabisa kwa sababu kuna mambo ya ukweli ambayo tumeyaonyesha.

"Tumefanya kila njia mpaka sasa hivi tumeshindwa, kwahiyo filamu ya Sister Marry haitatoka tena,” amesema Johari.