Tuesday, October 21, 2014

MUNGU MKUBWA APATA FEDHA KWENDA KUTIBIWA INDIA

MUNGU mkubwa! Ndiyo neno linaloweza kusemwa kwa  mrembo Zuhura Juma (27), mkazi wa Temeke jijini Dar anayesumbuliwa na uvimbe mguuni hatimaye Mungu amesikia maombi yake baada ya kupata msaada wa shilingi milioni 15 kutoka kwa Watanzania ambao waliochanga fedha hizo kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India.
Mrembo Zuhura Juma (27), mkazi wa Temeke jijini Dar anayesumbuliwa na uvimbe mguuni.
Kupitia Kampuni ya Global Publishers kwa mwandishi wake Imelda Mtema na Hoyce Temu wa Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten, harambe yao  walifanikiwa kukusanya fedha hizo ambazo zimetosha na sasa Zuhura ameondoka nchini jana kwenda India.
Akizungumza na mwandishi wetu, Zuhura alisema kuwa ana furaha isiyoweza kuelezeka kwani mateso aliyoteseka kwa nayo kwa kipindi cha miaka kumi yamefika tamati.
“Natoa shukurani zangu za dhati kabisa kwa walionichangia sina cha kuwalipa nitazidi tu kuwaombea kwa kuwa naamini kabisa ninaenda kupona ugonjwa ulinonisumbua kipindi cha miaka kumi,” alisema Zuhura.
Zuhura amesafiri kuelekea India katika Hospital ya Ganga iliyopo Mji wa Tamili Nadu chini wa daktari mahiri, Raja Sabapathy ambaye ndiye alifanikisha operesheni ya mtoto Hamis Hamza aliyekuwa na tatizo la mguu.