Saturday, October 18, 2014

Picha 5 za Majeruhi wa Moto Mbagala Dar waliolazwa hospitali ya Muhimbili

Majeruhi 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.
 
Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.
 
Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni  Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).
MAJERUHI
 
Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.