Tuesday, October 14, 2014

TASWIRA KUTOKA ENEO LA MBAGALA RANGI 3 BAADA YA LORI LA MAFUTA KUTEKETEA KWA MOTO NA KUUA

Moto ukiteketeza baadhi ya maduka yaliyokuwa jirani na lori la mafuta lililolipuka.
Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya moto huo kuzimwa.
WATU kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha kwa kuungua kwa moto uliolipuka wakati wakichota mafuta kutoka kwenye lori lililopata ajali usiku wa kuamkia leo eneo la Mbagala Rangi Tatu, Temeke jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa eneo la tukio ni kwamba watu hao walikuwa wakiiba mafuta baada ya lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta kupata ajali kabla ya kulipuka na kusababisha maafa hayo.
Mpaka sasa inadaiwa kuwa mtu mmoja amefariki katika ajali hiyo ila idadi kamili ya watu waliopoteza maisha bado haijafahamika.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hili zitaendelea kuwajia