Friday, October 3, 2014

UCHAKACHUAJI WA KURA KWENYE RASIMU YA KATIBA MPY!! ONYO KAMA HUJUIHESABU USISOME


Wajumbe  wa  bunge  la   katiba wakiwa  bungeni  dodoma

UCHAKACHUAJI WA KURA KWENYE RASIMU YA KATIBA HUU HAPA.!
**PRECAUTION: Kama hujui Hesabu usisome.!!
--------------------------
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi kuwa na kumbukumbu nzuri. Ukisema leo kuwa hujaoa halafu baada ya mwezi ukanikopa hela ili umtumie mkeo ni wazi kuwa utaumbuka.. Ukiamua kudanganya jitahidi kuwa na kumbukumbu sana (Liars must have a good memory).
Katibu wa Bunge Maalum leo katangaza kuwa jumla ya kura zote za Zanzibar ni 219. Japo Samuel Sitta alisema juzi kuwa wajumbe wa Zbar ni 210 but ngoja tukubaliane tu na Katibu kuwa ni 219 (hata km wamechakachua).
Kwa maana hiyo, theluthi mbili ya 219 ni 146. Na Theluthi moja ni 73.
Hivyo basi ili Rasimu ikwame kwa upande wa Zbar ilihitaji kura 74 au zaidi za kuikataa. Yani idadi yoyote ambayo itazidi 73 (theluthi moja) ingekwamisha Rasimu.
Wajumbe wa UKAWA kutoka Zbar ni 67, japokua wao wamesema ni 65 wakimaanisha wawili walipiga kura ya NDIYO. Tukubaliane nao kama tulivyokubaliana nao kwenye idadi ya wajumbe wa Zbar kuwa 219 badala ya 210.
Sasa twende kwenye Hesabu (Maths). Tuseme UKAWA walioikataa Rasimu ni 65 kama walivyosema. Ongeza 8 waliopiga HAPANA (wajumbe 7 plus Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aliyeikataa jana). Hadi hapo utapata kura 73.
Ongeza Abdallah Abbas ambaye aliondoka Bunge la Katiba na hakupiga kura. Jumla ni 74.
Hadi hapo tayari kura hizo zimeshazidi theluthi moja, ambayo ni 73. Lakini cha ajabu tunaambiwa Rasimu imepita. Imepitaje??
Kama waliokataa wamezidi theluthi moja, inakuaje tena waliokubali nao wazidi theluthi mbili? Hii hesabu mbona haipo? CCM wamechakachua wakashindwa kuweka hesabu vzr.!
Jamani chakachua kote lakini linapokuja swala la hesabu utaumbuka tu. Always number never lie.!
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!
BW ;  MALISA  GJ   -MWANDISHI   WA  MAKALA   HII


Read more: http://www.vitukovyamtaani.com/2014/10/uchakachuaji-wa-kura-kwenye-rasimu-ya.html#ixzz3F45bLeP5