Henda uliwahi kusikia kitu tofauti kuhusu ugonjwa aliokuwa anaumwa Rais Kikwete, jana Novemba 29 baada ya kuwasili Tz akitokea Marekani, alichokisema hiki hapa;
“… Operation imekwenda salama na madaktari wamefanikiwa kuyatoa maradhi yaliyokuwepo mwilini mwangu, yalikuwepo kwenye tezi dume… Sio maradhi ya busha… Akaja Proffesor mmoja akasema jawabu lake ni tufanye operation tu, afya yako ni nzuri ukiondoa hiyo utaishi miaka 30 inategemea umri wako Mwenyezi Mungu amekuandikia miaka mingapi…“– Rais Kikwete.
Nikasema kama nina miaka 30 huko mbele si haba lakini nitakuwa mzee mno nitakuwa nina miaka 94, au 95 huko nadhani sitakuwa na manufaa sana.. naweza kugeuka kuwa mzigo na matatizo kwa watoto na wajukuu mwishoni wakasema huyu babu hafi…”– Rais Kikwete.
Baada ya kulifahamisha Baraza la Mawaziri kwamba anaumwa, hali ilikuwa hivi;
“…Mheshimiwa Magufuli akaniambia Rais haagizwi lakini hivi kuna ubaya ukiambiwa kwamba Rais Baraza la Mawaziri linakuagiza kwamba usiseme?… Ni mmoja tu aliyekuwa ananiunga mkono nadhani mama Kabaka tu ndiyo alikuwa ananiuliza kwamba kwani kuna ubaya gani wa kusema, wengine wote wakasema wee nyamaza… Hakuna kusema… ” —Rais Kikwete.
Utaratibu ambao umezoeleka mtu anapofanyiwa operation ni wa kuchomwa sindano ya nusu kaputi, unadhani Rais Kikwete alifanyiwa hivyo pia wakati wa kufanyiwa upasuaji huo?
“… Wametia ganzi tu ile sehemu ya chini wanayotaka kufanya operation, wakaniambia unajua wewe Rais hatuwezi tukafanya uende ile kabisa nusu kaputi ulale usingizi, unaweza usiamke ikawa taabu… Nilipotoka pale naangalia eeh..! wameweka vyuma kabisa…“– Rais Kikwete.
Kidonda kile kimepona wametoa nyuzi lakini walichosema ni kwamba huku ndani wamekuchana sana kwa hiyo usidanganyike na unachokiona hapa juu kwamba pameziba lakini huko ndani bado mchakato unaendelea.. Wamesema mpaka miezi mitatu ndiyo kutakuwa kuna hakika…”
Hiki ndicho alichokisema kwa wale waliokuwa wakimuombea na waliokuwa wakimtumia ujumbe wa kumtakia heri na apone haraka;
Nitoe shukrani nyingi kwa Watanzania wote, walioniombea dua nipone.. Viongozi wa Dini na Madhehebu yote nimepata salamu zenu misikitini na makanisani mmekuwa mkiniombea nawashukuruni sana, nimepona… Mungu amesikia dua zenu na maombi yenu…”– Rais Kikwete.
Wako walionitumia sms kwenye simu zangu mpaka zikawa zimezidiwa mpaka tukafungua line maalum sasa.. Ile simu ilikuwa na message zaidi ya elfu tano, zimekuja mle watu wengi wakiwa wananiombea heri kwa kweli wote hao nawashukuru sana.. Ukipata sms zile ni kama vile watu wamekuja kukuangalia wodini pale…”– Rais Kikwete.