Na Mathias canal
Ndugu Zangu kuna wakati huwa najiuliza hawa watu wa Marekani ni kama wasukuma, maasai na wachaga maana nawaona maeneo mengi hapa Tanzania hususani katika misaada mbalimbali.
Lipo swali la kujiuliza hawa watu wa Marekani wamezaliwa mkoa gani ama ni wageni kutoka Marekani, yaweza kuwa wazawa lakini wamebobea kusaidia wazawa wenzao.(P.T)
La hasha hawa watu wa Marekani sio wazawa wa Tanzania bali wanashiriki katika kutuletea ufanisi wa misaada mbalimbali, hivi kwanini wanatusaidia kiasi kwamba hatujiwezi mpaka misaada ama ni sehemu ya kujenga urafiki na undugu lakini hata ujirani mwema pia.
Miaka kadhaa iliyopita watanzania hatukua na misaada kwa watu wa Marekani lakini kwa hivi sasa kila jambo wanasaidia wao haijalishi ni jambo kubwa au dogo tunapokea tu...
Naam kupokea misaada ni jambo moja vipi kuhusu sisi watanzania tutawasadia nini hawa Wamarekani ama wakipanda mlima Kilimanjaro wametosheka, au tutawapeleka Kalenga na Isimila watosheke.
Lakini hata Bagamoyo kuna Kaole wakiweza watafika, Kigoma kuna Gombe nayo vipi au Mikumi kuwatazama wanyama misutu yetu...Lakini vipi msaada ya Kimbaka(Tooth pic) wenyewe hawatupi bali hutengenezwa na Watu wa China wakati misitu kibao na mbao zake nyingi zipo Mufindi kwenye utata wa vibali lakini tunashindwa kutengeneza tu.
Hivi kipi bora kati ya kupokea ama kutoa, Dhahiri jibu jepesi ni kwamba heri kutoa maana ni moyo wakati utengano ni udhaifu...Mungu ibariki Tanzania tusiwe wadhaifu wakupokea pekee bali kutoa.
Hawa watu wa Marekani wanataka nini kwetu, hivi ni misaada pekee looooooooh, katika hesabu Mwalimu wangu alinambia ukijumlisha ujue kuna kutoa, lakini kugawanya kunaambatana na kuzidisha, isije kuwa wanafanya hesabu ya kutoa halafu wakati mwingine sisi tukajumlisha, kuzidisha na kugawanya(kugawa) kwa wakati mmoja...
Ni Neno La Wakati Mwema yawezakuwa kuna kabila No no no ni wageni rafiki zetu, Ndugu zetu na jamaa zetu wameongezeka Tanzania
Salaaaaaam