Monday, November 24, 2014

MTOTO ALIYEPEWA KIPIGO CHA KUFA MTU KUTOKA KWA HOUSE GIRL HUKO UGANDA, AFYA YAKE INAENDELEA VIZURI.

 
Mtoto akiwa hospitali anaendelea na matibabu Habari iliyo 'make' headlines kwa siku ya jana mpaka leo na imetokea kuisisimua jamii na kuiamsha kutoka katika usingizi fulani, habari juu ya mtoto aliyepata kipigo cha kufa mtu kutoka kwa house girl, kwa sababu kesi ipo mahakamani, hatuwezi kujaji sana ila tusubiri mahakama itoe tamko lake japo jamii imeshatoa hukumu kali kwa binti huyo hata tukiwa tunasubiri majibu ya mahakama. 

Kutokana na kipigo hicho, mitandao mingi iliripoti kuwa mtoto huyo kapoteza maisha kwa sababu ya kipigo kuwa "heavy" sana. Mtoto yupo salama na anaendelea na matibu.