Monday, November 10, 2014

NDOA YA MBONGO MOVIE JACK PENTZEL.. SASA KIMENUKA KWELI KWELI

NDOA ndoano ! Staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Steven Pentzel ‘ Jack Pentzel’ na
mumewe Gardner Dibibi wanadaiwa
kukinukisha na kuingia kwenye gogoro la kila
siku hadi mwanaume kutaka kuondoka
nyumbani wanakoishi Mbezi - Shamba jijini
Dar.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Steven Pentzel ‘ Jack Pentzel ’ akiwa na
mumewe Gardner Dibibi .
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo
makini ambacho ni mtu wa karibu wa
wanandoa hao, kilisema kwamba, kila kukicha
wawili hao wamekuwa wakigombana na
sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi
nyumbani.
Ilidaiwa kwamba, tangu Jack awe na ushosti
na staa mwenzake wa sinema za Kibongo,
Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na
kujisahau kwamba ni mke wa mtu . “ Yaani
ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila
siku wanapigana na hivi karibuni mumewe
alikusanya nguo na kuweka kwenye begi
akitaka kuondoka nyumbani .
“ Tatizo mwanamke anachelewa kurudi
nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo
mgogoro unaanzia hapo, ” kilisema chanzo
hicho. Baada ya kunyetishiwa ‘ ubuyu’ huo ,
Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack,
Dibibi ili kueleza ukweli juu ya suala hilo.
‘ Jack Pentzel ’ na mumewe wakiwa kwenye
picha ya pamoja na Rose Ndauka .
“ Kutofautiana ni jambo la kawaida na huwa
tunagombana tu kawaida lakini siyo ugomvi
mkubwa kama watu wanavyosema.
“ Sijaondoka nyumbani, mbona nipo tu na mke
wangu, hao wanaosema hivyo wanataka
kutukosanisha tu . ”
Kumekuwa na uvumi wa kuvunjika kwa ndoa
hiyo iliyofungwa mwanzoni mwa mwaka jana
ambayo haijajaliwa kupata mtoto.