Monday, November 17, 2014

POMBE SIO CHAI:BINTI WA KIARABU ALEWA, AFANYA VIOJA NA KUACHA MAMBO HADHARANI

POMBE si chai! Binti mrembo mwenye asili ya Kiarabu ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akifanya vioja baada ya kulewa chakari na kusababisha midume kumtolea udenda, Ijumaa Wikienda lilimpiga chabo.
Binti huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja akifanya yake.
Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye onesho la Kundi la Mashauzi Classic ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo lilikuwa likitambulisha albam yake mpya ya Sura Surambi, Sura Siyo Roho.
...Akizidi kuserebuka ndani ya ukumbi huo.
Awali binti huyo alionekana ukumbini humo akiwa mpole na mwenye sura ya soni huku akipata kilaji polepole kabla ya kumkolea na kuwa staa wa kubinuka kihasarahasara na kumwaga ‘lazi’ mbele ya kadamnasi huku akiacha sehemu ya maungo yake nyeti kweupe.
“Jamani pombe mwanaharamu. Muone yule binti wa Kiarabu, kaja mpole lakini hebu ona vituko utadhani kuna skruu imefunguka kichwani,” alisema mmoja wa mashuhuda.Katika hali iliyoonekana kuzidi kuelemewa na kilaji, binti huyo alianza kuwavaa wanamuziki stejini na kuwakumbatia kisha kuinua mguu na kurusha mateke ya kinyumenyume kama mwanasoka, Cristino Ronaldo wa Real Madrid.
Vioja vya binti huyo havikuishia hapo kwani aliwavaa wanaume na kuwakatikia vilivyo.
Wakati tukio hilo likiendelea, jamaa mmoja alimfuata akidai ni mkewe ambapo alimfokea mwanahabari wetu akimtisha kwamba endapo akiziona picha gazetini atamfanya lolote akafie jela Segerea.