MSHTUKO! Kifo cha Askofu na Nabii wa Kanisa la The Pool of Siloam lililopo Mbezi-Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam, Elia Munuo almaarufu kwa jina la Adam wa Pili, Mungu wa Majeshi, kimeacha ‘sintofahamu’ kwa kuwa kiongozi huyo alitabiri na kutangaza tukio hilo na likawa kweli, Ijumaa Wikienda limechimba undani wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni viongozi na baadhi ya waumini wa kanisa hilo, tukio hilo lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo askofu huyo aliwaita makuhani (Viongozi) kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bongo na kuwaambia mambo manne muhimu.
Mambo hayo ni pamoja na wosia wake ukiwa na kauli yake ya kusindikiza safari yake ya mwisho kwa kuwa alikiona kifo chake kuwa kingejiri mchana wa siku hiyo na kuwataarifu huku akiwa mzima wa afya.
Kwa mujibu wa msemaji wa kanisa hilo, Kuhani, Kiongozi Miaka 1,000 aliwaambia kuwa amekamilisha kujenga msingi wa kanisa la mwisho la kizazi cha nne.
Kwa mujibu wa msemaji wa kanisa hilo, Kuhani, Kiongozi Miaka 1,000 aliwaambia kuwa amekamilisha kujenga msingi wa kanisa la mwisho la kizazi cha nne.
Alifafanua kwamba, baada ya miaka 1,000 ya kanisa, walianza mwaka wa kwanza ambapo alitambulisha tarehe ya Kimungu (Kirumi) kwa maana hiyo yeye alifanya kazi ya utumishi kwa miaka 12 na hatimaye aliikamilisha.
“Alifanya kazi kwa muda wa miaka 12 hadi anatwaliwa lakini kwa kawaida hatuna mwaka wa kumi na ukiangalia miaka yetu tunaanza na 1-9, halafu tunaanza tena na moja hivyo nabii wetu alikuwa kwenye uongozi kwa mwaka wa tatu kabla hajatwaliwa na Mungu,” alisema Kuhani.
Lango kuu la kanisa hilo.
Miongoni mwa kile kinachozungumzwa juu ya tukio hilo na kuacha viulizo kwa makuhani hao ni baada ya kuwaambia kuwa, gari lake lilikuwa linakuja kumchukua mchana wa siku hiyo bila wao kuelewa alichokuwa akimaanisha kwa ufasaha.
Hili liliacha viulizo sana kwa sababu gari lake alimaanisha kuwa ndicho kifo chake na katika miujiza kweli akafa mchana huo.
“Kusema kweli hili kanisa lina bahati sana. Elia tulikuwa naye hapa japokuwa amekwenda, lakini tumebaki naye kiroho. Tunaamini atarudi kama Yesu,” alisema kuhani huyo.