Tuesday, December 16, 2014

AFYA: HIZI NDIO FAIDA NNE ZA KULA CHOCOLATE KILA SIKU...SOMA HAPA

30311-chocolate-zone-chocolate-bars
 Katika hali ya kawaida watu wengi huambiwa kuwa Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa chocolate si nzuri.

Wengine husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa inasababisha kisukari na wengine huenda mbali wakidhani kuwa inaharibu ngozi kutokana na wingi wa mafuta.
Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi wao katika hili.
Ukweli ni kwamba Chocolate sio mbaya kwa afya yako na hii sio story bali ni matokeo ya utafiti rasmi ambayo yamekuja na sababu hizi nne ambazo ukishazisoma hautakosa chocolate kwneye maisha yako walau hata mara tatu mpaka tano kwa wiki.
1.Chocolate ni nzuri kwa Moyo wako.
Utafiti unaonyesha kuwa chocolate inaweza kusaidia kupunguza magonjwa ya moyo n ahata shinikizo la damu na shambulio la moyo au Heart Attack.
Chocolate nyeusi zimethibitika kuwa na uwezo wa kusaidia moyo ambao umeanza kuathirika na matatizo ambayo yanaweza kukuletea ugonjwa wa kiungo hicho muhimu kwenye mwili wa binadamu.
 chocolate-bar

2.Inapunguza kisukari.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli halisi ni kwamba , chocolate inasaidia kuondoa uwezekana wa mtu kupata kisukari.
Watu ambao wamekuwa na kawaida ya kula chocolate walau kipande kidogo mara moja kwa siku kwa muda wa siku tano wanakuwa na uwezo wa kuwa na kinga dhidi ya kisukari kuliko wale ambao hawali chocolate kabisa.
3.Kupambana dhidi ya Msongo wa mawazo.
Tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa chocolate inasaidia kupunguza msongo wa mawazo au stress.
Watu wenye  msongo wa mawazo hushauriwa kula walau gramu 45 za Chocolate kila siku wa muda wa wiki mbili ili kushusha msongo wa mawazo.
Chocolate hushusha kiwango cha Homoni ya Cortisol mwilini, homoni hii huongeza au kupunguza msongo wa mawazo.
4.Chocolate husaidia kujikinga dhidi ya Jua.
Ni vigumu kuamini lakini chocolate husaidia ngozi ya mawadamu kujikinga dhidi ya madhara ya miale ya jua.

Flavonoids ambazo zinatumika kutengeneza chocolate zina chembechembe ya vimelea vinavyoweza kusaidia ngozi na kuikinga dhidi ya miale ya jua.