Tuesday, December 16, 2014

Meseji ya Kwanza Kutoka Kwa Miss Tanzania Happiness Kwenda kwa Watanzania Wote Baada ya Shindano Hilo Kwisha Hapo Jana

Baada ya Miss South Africa anajulikana kwa
jina la Rolene Strauss ambaye ndie mshindi
wa taji la Miss World 2014, Aliyekuwa
akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo
kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram
amefunguka baada ya kushindwa kunyakua
taji hilo na hichi ndicho alichokiandika:
Nampongeza @rolenestrauss (South Africa)
kwa kuibuka mshindi Miss World
2014.Watanzania wenzangu na marafiki kutoka
mataifa mengine, tumepiga kura sana,
mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio
ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha.
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja
mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi
chote ambacho nilikua hapa jijini #London na
tokea niliposhinda mashindano ya
#MissTanzania. Nisingefika hapa bila support
yako. From deep inside my heart. I thank you.
Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake
kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza
habari yangu, designers mbalimbali, familia
yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you.
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki
na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja
wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu
katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa
letu.
Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld
Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22
akiwa ni mwanafunzi wa chuo cha udaktari
katika chuo kikuu cha Free State (University of
Free State) Rolene alifuatiwa na mshindi wa
pili amabye jina lake ni Miss Hungary Edina
Kulcsar.