Makundi ya mashabiki mitandaoni maarufu kama
TEAMS yamekuwa ni sehemu ya maisha ya
mtandaoni ya wasanii na watu maarufu wengi
hapa nchini. Linapokuja swala ya ushabiki na
mada nzito team hizi huvutana kwa kutupiana
maneno na wakati mwingine hadi maneno makali.
Siku za hivi karibuni baada ya mwigizaji Wema
Sepetu alipoachana na mpenzi wake Diamond
Platnum, na badaye Diamond kuamua kutoka na
mwanamama Zari kutoka nchini Uganda,
Mashabiki (TEAM) wa Diamond na wale
wanaomponda Wema Sepetu wamekuwa kwakiasi
kikubwa wakiwatupia maneno na vijembe wale
mashabiki wa Wema (TEAM WEMA), kwa picha na
maneno.kiasi ambacho TEAM WEMA kuonekana
kama” LOSSERS”.
Lakini leo hii upepo umebadilika huko mitandaoni
na TEAM WEMA wanaonekana kuwa na nguvu
zaidi, baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuachia
baadhi ya picha akiwa nchini Ghana akifanya kazi
na Van vicker ambae ni msanii mkubwa hapa
Afrika.