Thursday, December 11, 2014

BELA AKANUSHA SKENDO YA KUMUUA MWANAMZIKI WAKE

STAA anayewika na Ngoma ya Nani Kama Mama, Christian Bella ‘Obama’ ameibuka na kupangua tuhuma za kumuua mwanamuziki wake, Adaya aliyeaga dunia hivi karibuni kabla Bella hajaenda kufanya muziki nje ya nchi.

 
Staa anayewika na Ngoma ya Nani Kama Mama, Christian Bella ‘Obama.

Akipiga stori na Amani baada ya kuulizwa shutuma hizo Bella alifunguka, kuwa yeye hajui mambo ya uchawi wala hajawahi kuua mwanamuziki wa aina yeyote. “Watu wanajua kuongea tu ina maana hata huyo Diamond alivyo juu kwa sasa ameua mtu?, basi kama ushirikina wa aina hiyo ungekuwepo mastaa wengi wangekimbilia huko na kuua wenzao,” alisema Bella.
Aidha Bella alisema kuwa yeye anavyojua mwanamuziki huyo alifariki baada ya kuugua na alianzia kuumwa Mwanza kwa ndugu zake.