Sunday, December 28, 2014

CHECK PICHA NNE ZA MTOTO ZA KAJALA ..... YAANI NISHEEDAAH





Upendo wa mama kwa mtoto wake hauwezi kufananishwa na kitu chochote hapa duniani,kwa hili nadhani hakuna anaebisha.Ila ni ukweli pia wazazi  hutofautiana katika kuonyesha mapezi kwa watoto wao,hapa nazungumzia mahusiano ya wazazi na watoto katika maisha ya kila siku.

Kwa sisi watoto wa maika ya 1980+ wazazi wetu wengi walitufanya tuwaogope na kuwaheshimu hata kwanidhamu ya woga, kitu ambacho mimi nakipinga sana.Leo mambo ni tofauti sana, wazazi wengi wamekuwa wakijitahidi kujenga urafiki na watoto wao na hivyo kuleta ukaribu na uwazi baina yao, kitu ambacho ni kizuri zaidi kwa ulimwegu huu wa sayansi na tekelinalokuijia.

Turudi kenye mada
Kama umekuwa ni mtu kumfuatilia mwigizaji Kajala Masanja, naamini utakubaliana na mimi kuwa  Kajala na binti yake Paula, bali ya kuwa na mahusiano ya  mtu na mtoto wake lakini wanaishi kama mtu na rafiki yake.

Hiki kitu huwa kinanikosha sana, kwani naamini hii uongeza  ukaribu na upendo baina yao,pia inatoa fursa ya mtoto kuwa muwazi kwa mzazi wake.

 Mara zote wamekuwa wakionekana kuwa pamoja kwenye hali zote, furaha nahata udhuni.Naamini katika malezi ya namnahii hutoa nafasi kwa mzazi na mtoto kuzungumza kwa uwazi na kushauriana katika jambo lolote.

Hongera sana Kajala kwa kutuonyesha hili,naamini wengi watajifunza kupitia wewe, kwangu wewe ni mama na mlezi bora zaidi kwa mwaka huu.