Msanii wa filamu, Mahsein Awadh Said aka Dr. Cheni’ amesema filamu yake ya ‘Nimekubali Kuolewa’ iliyokuwa imezuiwa kutoka na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inatarajiwa kutoka mapema mwakani baada kukamilisha matakwa yao.
Dokta Cheni alisema kuzuiliwa kwa filamu hiyo kulimnyima raha kiasi cha kumfanya asifanye kazi nyingine mpaka akamilishe kazi hiyo.