Mwigizaji wa filamu,mrembo na mwenye mvuto wa kufanya wengi wapagawe, Elizabeth Michael aka Lulu ambae kwasasa yupo Mjini Bukoba kwa mapumziko mafupi. Akiwa katika viwanja vya kula bata mjini hapo Lulu hakusita kuwasifia watu wa kabira la Wahaya kwa njinsi alivyo furahia GOOD TIME alilopewa na kumfanya afunguke mwenyewe kwenye mitandao ya kijamii
“Wahaya noma......
Hili Bata la Watu wa Bukoba ni Noumer...! likizo isiishe jamani”
Haikuishiahapo, alitupia picha nyingi mtandaoni akiwa "SAMUWEA" kama unavyoziona hapo juu. Lakini hiyo picha ya miguu ndio iliua wengi, kwakuitendea haki alifunguka.
“Nishawahi kusema naipenda miguu yangu!????
Wallah Naipenda kwa Moyo mmoja ,oky naendelea kuoga hela..kuoga Maji mwisho Dar Es Salaaam...kwa kina Mutashobya(BUKOBA) ni kuoga Hela tu...!oky bye” Lulu alimaliza.
Picha zote hapo juu. Bongomovies.com inamtakia likizo njema na arejee Dar es salaam salama.