Thursday, December 25, 2014

MADAI MAZITO ROSE NDAUKA, RICHIE WARUDIANA

Staa  wa sinema Bongo, Rose Ndauka akifurahia jambo.
Na Waandishi Wetu
MASTAA  wa sinema waliowahi kuwa wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa kurudiana na hivi sasa ni mapenzi motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose na Richie wamedaiwa kurudiana baada ya mwanadada huyo kumwagana na mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi ya hivi karibuni.
“Hivi nyie wadaku mnajua Rose Ndauka na Richie sasa hivi ni mahaba niue kama zamani? Wamekuwa wakigandana na mara nyingine hupatikana maeneo ya Bahari Beach (jijini Dar) kiasi kwamba wasanii wenzao tunawashangaa.
“Inaonekena walipomwagana hakuna aliyekuwa tayari,” alisema msanii mmoja wa filamu za Bongo ambaye aliomba jina lake kusokomomezwa kwenye makabrasha ya gazeti hili.Baada ya kuzinyaka habari hizo, Amani lilimtafuta Richie kwa njia ya simu ya mkononi  ili aeleze chochote  kuhusu madai hayo.
Staa wa sinema Bongo, Single Mtambalike ‘Richie’ akipozi.
“Unaposema tumerudiana una maana gani? Mimi sijawahi kuwa na uhusiano na Rose Ndauka itakuwaje sasa turudiane? Hakuna kitu kama hicho, mimi na Rose tulikuwa tunacheza filamu ambayo nilimshirikisha na tumemaliza.
“Halafu sikia wewe, mimi si mtu wa magazeti na endapo mtaandika hii habari nitamfanyia mtu ‘kitumbaya’ hadharani maana ninyi mnatafuta habari za uongo ili mpate fedha.”
Baada ya Amani kumalizana na Richie, lilimsaka Rose Ndauka ambaye naye aliruka kimanga:
“Ha! Ha! Mimi sijarudiana na Richie, tulikuwa tunacheza filamu moja ndiyo maana muda mwingi tulionekana kuwa wote. Lakini filamu yenyewe tumeshamaliza.”