Thursday, December 25, 2014

MAMA KANUMBA: KRISMASI KWANGU NI MBAYA

Flora Mtegoa ambaye ni mama wa marehemu Steven Kanumba.
Na Laurent Samatta
FLORA Mtegoa ambaye ni mama wa marehemu Steven Kanumba, amesema kuwa Sikukuu ya Krismasi kwake imekuwa mbaya kutokana na kifo cha mama yake mzazi kilichotokea mwaka huu tarehe na mwezi aliyofia Kanumba.
Akizungumza na Amani, mama Kanumba alisema kuwa anashindwa kuelewa ni kwa nini matatizo kwake yanakuja siku ambayo mwanaye Kanumba alifariki kitu ambacho kinampa wakati mgumu hadi akili yake inashindwa kufanya kazi.
“Siwezi kusema nina furaha wakati mama yangu hayupo na hiyo ndiyo inayonipa wakati mgumu wa kutokuwa na furaha kwenye maisha yangu, nina majonzi ya muda mrefu pengine Kanumba angekuwepo basi ningeweza kula kwa amani,” alisema.