Thursday, December 25, 2014

KIVAZI CHA SHILOLE CHAZUA UTATA

Staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Shani Ramadhani
STAA wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amezua utata kufuatia kivazi alichopigilia usiku wa siku ya bethidei yake iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Baraka Plaza, Mikocheni jijini Dar.
Kivazi hicho alichokuwa amekivaa Shilole, kilikuwa kimeacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake jambo lililozua mjadala kwa watu kutokana na wahudhuriaji wengi wa kiume kumtolea macho na kuishia kusema;
“Nuhu amejipatia mke mzuri sana, sasa cheki nguo aliyovaa, kiukweli anatutia majaribuni mwanamke huyu ana kusudi jamani mmmh... inatakiwa amdhibiti kwa sababu yeye ni mwanaume ana maamuzi pia vinginevyo mwana atakuwa si wake maana wapo mapedeshee wanam-kodolea macho.”