Sunday, December 14, 2014

Mshindi wa Pili wa BBA Hotshots 2014: Akanusha kupewa pesa na tajiri wa Nigeria

Mshindi wa pili wa BBA Hotshots, Tayo kutoka
Nigeria amekanusha ripoti zilisambaa wiki hii
kuwa amezawadiwa $350,000 na bilionea wa
Nigeria baada ya kuzikosa $300,000 za BBA
zilizonyakuliwa na mshindi wa kwanza mwaka
huu Idris wa Tanzania.
Ripoti hizo zilidai kuwa Tayo alipewa zawadi
hiyo na bilionea aitwaye Ayiri Emani kama
kifuta jasho au fidia ya kuzikosa $300,000 za
mshindi wa HotShots.
Tayo amekanusha habari hizo alipohojiwa na
kituo cha Radio 1 South Africa. Amesema
kuwa habari hizo za kuwa amepewa kiasi
hicho kikubwa cha pesa na huku hata
hamfahamu bilionea huyo, zimemletea
usumbufu kwasababu watu wengi watadhani
yeye ni milionea na huku sio kweli.
Tayo aliongeza kuwa yeye na Idris ni marafiki
na anatarajia kuja Tanzania mapema
iwezekanavyo.
Chanzo: Big Brother Africa 2014