Sunday, December 14, 2014

Unajua kilichofanywa na Mtazamaji baada ya kukerwa na vazi la Mtangazaji?

TV studio with camera and lights
Iwapo mtu anakuwa mtangazaji wa TV halafu ni mwanamitindo kuna namna ambavyo biashara zake zote mbili zikawa zinabebana, labda ndicho kilichomfanya avae nguo ambayo aliona itaonekana vizuri mbele za watu waliokuwa wakiangalia show ya TV ilipokuwa ikirekodiwa lakini kumbe kuna ambao hawakupenda hivyo.
Mtangazaji huyo Gauhar Khan hakutegema hili, limemkuta akiwa anarekodi sehemu ya mwisho ya show ya TV huko Mumbai, ambapo alitokea mtu mmoja Akil Malik na kumpiga kibao usoni na kusema kwamba Khan hakuvalia vazi sahihi kutokana na utamaduni wao kwani sketi yake ilikuwa fupi sana.
Haikuwa rahisi, Malik aliweza kukabiliana na walinzi zaidi ya mia mbili waliokuwa ndani na nje ya studio na  kuingia ndani ambapo alifanikisha lengo lake.
Jamaa huyo alikamatwa na kupandishwa kizimbani huku Khan akilazimika kurudisha ile mood ya kazi na kumalizia show hiyo japo alikuwa kwenye wakati mgumu bado kurudi kwenye hali ya kawaida.
Mkasa huo uko kwenye video hapa.