Sunday, December 28, 2014

USIKU WA USWAZI NA WASWAZI NI NOMAAA DAR LIVE

Msanii Inspector Haroun akiimba na mashabiki wake.
Chid Benz kavua shati baada ya mzuka kumpanda.
Mesen Selekta akiimba kanyaboya pamoja na wacheza shoo.
MC na Muimbaji, Pam D akizungusha nyonga.
Mnyama, TID akiwa na kimwana stejini.
Kundi la Umeme wakifanya yao stejini.
Kala Pina akikumbushia ngoma za kitambo.
Wabibi wakikamua.
Kundi la Yakuza Mobb wakikamua.
Wadau wa muziki wakiwa stejini.
JANA katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, wasanii kibao wamedondosha bonge la shoo katika Usiku wa Uswazi na Waswazi, shoo iliyoandaliwa na Defatality Music ikiwashirikisha mastaa wakongwe kama Chid Benz, Top in Dar ‘TID’ ,Yakuza Mobb, Kalapina, aka “Mbuge Mtarajiwa’’, Pam D pamoja na wasanii kibao wanaokuja kwa kasi wakiwemo Kundi la Umeme na Wabibi.
Wasanii wengine waliodondosha burudani ni pamoja na Kala Pina aka ‘’Mbunge mtarajiwa’’ Top in Dar ‘TID’, Kundi la Umeme, Inspector Haroun, Yakuza Mobb, Mesen Selekta, Pam D na wengine kibao.