Friday, December 19, 2014

VIDEO: ANGALIA MH TIBAIJUKA ALIVYOSISITIZA HATOJIUZULU MBELE YA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka, jana alikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la Akaunti ya Escrow, huku akisema haoni sababu ya yeye kujiuzulu kutokana na kudaiwa kuhusika katika sakata hilo.
Alisema hawezi kufikia uamuzi wa kujiuzulu kwa kuwa hana kosa kwani hajatajwa mahala popote katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG ), ingawa hakupewa nafasi ya kujitetea na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).Video: Angalia Mh Tibaijuka Alivyosisitiza Hatojiuzulu Mbele Ya vyombo Vya Habari
Alisisitiza fedha alizopewa na Rugemalila ni mchango wa Shule ambapo alisema lengo lake kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.
Alipoulizwa kuhusu kujiuzulu alisema hawezi jiuzulu kwani haoni sababu ya yeye kujiuzulu.