AFIKISHWA POLISI NA WANANCHI BAADA YA KUWATAPELI MAMILIONI KWA KUJIFANYA AFISA WA WAKALA WA UMEME VIJIJINI
Wananchi wa kijiji cha kurwaki wilayani Butiama mkoani Mara wamemkamata na kumfikisha katika kituo cha polisi cha mugango wilayani humo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwatapei baadhi ya wananchi kwa kujifanya kuwa ni afisa wa wakala wa umeme vijijini rea huku akidaiwa kukusanya mamilioni ya fedha kutoka kwa wananchi kwa lengo la kuwaunganishia nishati ya umeme katika nyumba zao.