Filamu mpya inayofananishwa na ile ya Expendables ya nje ya nchi lakini sasa hii ya kitanzania imepewa jina la WAKE UP wakati wa kuigizwa kwake ilikumbana na majanga makubwa kufuatia mastaa wake kurumbana na hata kununiana huku wakirekodi filamu hiyo ya msanii Manaiki Sanga.
Muongozaji wa filamu hiyo Leah Richard Mwendamseke “Lamata” alisema kuwa filamu hiyo ilikuwa na majanga makubwa sana hadi kuja kumalikia kufuatia mastaa wengi kuleteana ubabe wakati wakiigiza.
Lamata aliendele kusema kuwa uigizaji wa filamu hiyo hadi kukamilika umechukua miezi sita huku wakipambana majanga makubwa" Kaka haikuwa rahisi kuwaweka mastaa wote hao zaidi ya 30 pamoja kwa miezi sita ilikuwa shughuri sana na ilipelekea wakati nilikuwa nafaunga na kusali ili nimalize filamu ya watu" Alisema dada huyo
Hata katika tukio la wazi ni lile ya msanii Hemed kutaka kumpiga makosi ya kweli msanii Irene Uwoya wakati wakiigiza sini yao na kupelekea kusimama kwa muda kupisha ugomvi huo kwa wasingeweza kuendelea kurekodi wakati hawako kwenye mudi nzuri,
Filamu hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua za mwisho kumalika huku makampuni makubwa ya usambazaji yakipigana vikumbo kupanda dau wasanii baadhi waliogiza ni Irene Uwoya, Jackline Wolper, Gabo, Othuman Amri “King Majuto” Kajala, Yusuph Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed Suleiman, Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul, Flora Mvungi, kwa upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B akiwemo mwenyewe Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa filamu hiyo.