Friday, January 2, 2015

ASHA BARAKA AMUONYA DIAMOND KWA UNGA

Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka amemuonya msanii anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutojaribu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusema akijaribu atapotea.
Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.
Akizungumza na Ijumaa hivi karubini, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema Diamond anaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi inayokuja lakini akijaribu kutumia dawa hizo ataishia pabaya.
“Tumeona wasanii wengi wa Tanzania ambao awali walikuwa wanafanya vizuri lakini baada ya kujaa sifa na kukutana na marafiki wengi pamoja na makundi wakazama kwenye dawa za kulevya na sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu wakati wenyewe wamejiharibia,” alisema Iron Lady.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Wasani ambao awali walikuwa wakifanya vizuri kimuziki lakini baadaye ‘wakadrop’ baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya unga ni pamoja na Chid Benzi, Ray C, Q Chiller, Lord Eyez, Msafiri Diof na wengine ambao sasa wameshafariki.