WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti kwa nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.
Nyota wa filamu na muziki, Baby Madaha.
Akizungumza na Uwazi, Madaha alisema kuwa hajui kifo chake kitatokea lini na anachotaka ni kutimiza yale aliyopewa kama wosia na marehemu baba yake ambaye alizikwa jijini Mwanza. “Nasema ukweli sitaki kuzikwa Dar hasa kwenye makaburi ya Kinondoni, nahitaji kupelekwa nyumbani, wasanii wenzangu wanatakiwa kujua hilo pamoja na ndugu zangu pia, naamini kwamba marehemu baba yangu huko aliko ataona ni vizuri mimi kulala karibu yake kama alivyoniachia wosia huo,” alisema Madah