Monday, January 5, 2015
CHRIS BROWN AWA GUMZO KWA MUONEKANO WAKE MPYA 2015!!
Jana tulikuletea story kuhusu mtindo mpya wa nyewele wa Joti ambao uko tofauti kabisa na nywele zake zilivyowahi kuwa hapo nyuma.
Joti si star pekee aliyeanza mwaka 2015 akiwa na style mpya ya nywele, mkali wa miondoko ya R&B Chris Brown naye ameamua kuja na style ya tofauti ya nywele ambayo hajawahi kuwa nayo.
Style Mpya ya Nywele ya Chris Brown inaonekana hivi.
Breezy ameamua kusokota rasta ndogo ndogo na kuachana na ile style yake iliyozoeleka ya kunyoa nywele fupi ya Lowcut ambayo kila mmoja ameizoea.
Hapo awali Brown aliwahi kuwa na style ya kuweka rangi ya dhahabu au blonde style ambayo ilimfanya aonekane tofauti na mwanzoni wakati nywele zake zilipokuwa fupi na nyeusi.
Moja ya mtindo wa nywele ambao Chris Brown aliwahi kuwa nao ni huu wa kupaka nywele zake rangi kama hivi.
Kabla ya kuwa anapaka rangi nywele zake zilikuwa hivi.
Mwanzoni wakati anatoka Chris Brown alikuwa na nywele za chini ‘Lowcut’.