Tukiwa ndio tuanaunza mwaka huu wa 2015, tegemea kazi mpya kutoka kwa mwigizaji mahili kabisa wa filamu hapa nchini, Riyama Ally ambae kwa sasa yupo katika hatua za mwisho kuikamilisha kazi hiyo.
Filamu itakwenda kwa jina la DAMWANI ambayo itakua inahusu maswala ambayo yapo kwenye jamii yetu kwenye maisha yetu ya kila siku, filamu hii imejumuisha waigizaji wakongwe na wachanga na wageni kwenye tasnia hii ya filamu hapo bongo.
Akionekana mbele ya kamera,Riyama akiwa na mwigizaji mwenzie aliweka mtandaoni picha hiyo hapo juu nakuandika;
“MUNGU WANGU bariki kazi ya mikono yetu amin # Kazini damwani”Haijaahamika ni lini hasa kazi hii itatoka lakini lazima itatoka ndani ya mwaka huu.Tukae mkao wa kula