Saturday, January 31, 2015

JINI KABULA AMTAKA CHUZ AOE

Mwigizaji aliyekwenda hewani Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amemtaka mzazi mwenziye, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ aoe ili kulinda heshima yake.
Mzazi mwenza wa ‘Jini Kabula’, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ akipozi.
Akizungumzia maisha yake ya uhusiano mbele ya mwanahabari wetu, Kabula alisema anajivunia kuzaa na Chuz lakini kwa kuwa yeye hakupanga kuolewa na prodyuza huyo mkongwe, ni bora aoe kwani umri unamtupa mkono.
“Chuz aoe tu sasa umri umeenda. Tena akioa  mimi nitacheza muziki balaa siku hiyo, si unajua mambo yangu. Mbaya zaidi sina kabisa wivu naye,” alisema Jini Kabula.