Saturday, January 31, 2015

MAFUFU AMSHUSHA RADO GARINI

MWIGIZAJI Jimmy Mafufu amenaswa akimshusha kwa nguvu mwigizaji mwenzake Rado alipomuomba lifti ya kwenda Kariakoo wakitokea Mwanyamala, Demag Hotel.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Jimmy Mafufu.
Paparazi wetu alimshuhudia Mafufu akimshusha kwa nguvu Rado kwenye gari lake aina ya Toyota Passo kwa kile alichodai hayupo tayari kumpakiza kwani hajui kwenye gari hilo jipya ameweka nini.
“Shukashuka, bora apande mwingine kuliko wewe,” alisikika Jimmy huku Rado akitii amri bila shuruti na kuondoka.