MTOTO wa kwanza wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Fidel Odinga amefariki dunia leo alfajiri akiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika. Raila Odinga amethibitisha kifo hicho.
Fidel alikimbizwa hospitali na mkewe baada ya kuwasili nyumbani majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na kulalamika kuwa anapata shida katika upumuaji.
Fidel na baba yake Raila, jana mchana walipata chakula cha mchana pamoja na kiongozi huyo wa Cord ameeleza leo asubuhi kuwa kijana wake hakusema kama ana tatizo lolote la kiafya. Baadaye jioni marehemu alitoka na marafiki zake ambapo alirejea nyumbani saa 7 usiku na kudai kusumbuliwa na tatizo la upumuaji.