Thursday, January 8, 2015

MWANAMKE ALIYEPEWA UPADRI YUPO HATARINI KUTENGWA NA KANISA KATORIKI!

padri2 
Pamoja na kwamba sheria za kanisa Katoliki haziruhusu mwanamke kuwa padri lakini mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Georgia Walkeramepewa cheo cha upadri katika jimbo la Kansas nchini Marekani,tukio ambalo ni la kwanza kwa kanisa katoliki.
 Mwanamke huyo mwenye miaka 67 ambaye awali alikuwa sista alipewa daraja hilo jumamosi iliyopita lakini upadrisho wake uliingia kwenye mzozo baada ya uongozi wa kanisa lake kudai hautambui kuapishwa kwake.
 tayar 
Kutokana na hatua hiyo sista huyo anaweza kutengwa na kanisa kutokana na ukweli kuwa sheria za kanisa zinasema mwanamke hawezi kuwa padri.
 Lakini kwa upande wake alipingana nao na kusema haoni sababu za kukataliwa kuwa padri kwani Yesu alifundisha watu wote bila kubagua jinsia wala hadhi zao.
 Ibada ya upadrisho iliongozwa na Askofu Bridget Mary Meehan wa Chama cha Mapadri wanawake wa kanisa Katoliki na wakati akipewa upadri hakuonyesha hofu yoyote mbali na tishio lakutengwa na kanisa.