Sunday, January 25, 2015

NI KWELI UMAARUFU WA WEMA SEPETU UMESHUKA BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND?

Miaka kadhaa iliyopita, Diamond Platnumz alikuwa kijana mwenye ndoto kama underground wengine wa muziki walivyo na hasira ya kutoka.

Kutoka kwenye familia ya kawaida (kama zilivyo familia nyingi za Kitanzania), Diamond alikuwa akihaha huku na kule kutafuta fedha ya kuingia studio.

Fast forward – kwa kuungaunga hivyo hivyo alifanikiwa kurekodi wimbo uliokuja kubadilisha maisha yake, ‘Kamwambie’.

Ni wimbo aliouandika kwa hisia kutokana na kuhusisha kisa cha kweli cha kuachwa na msichana. Ni kipindi hiki ambacho ‘Kamwambie’ inafanya vizuri ndipo mapito ya Diamond na Wema yaligongana.

“Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Bilicanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili,” Wema aliiambia Bongo5 mwaka juzi.

“Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani.”

Na kweli kwa kipindi hicho, pamoja na kuanza kuwa na jina kubwa, Diamond alikuwa bado hajaupgrade swagga zake huku Wema Sepetu akiwa kwenye kipindi ambacho kila mwanaume alikuwa na ndoto ya kuwa naye.

Kwa maana nyingine kipindi hicho Wema alimuona kama mtu asiye na hadhi ya kuwa naye.

Fast forward tena – baada ya kuachana na Chaz Baba, Diamond na Wema wakawa wapenzi. Ikawa couple moja yenye nguvu sana japo ni Wema ndiye aliyekuwa na nguvu zaidi kuliko mwenzie.

Pamoja na kuendelea kutoa hits mfululizo ikiwemo ‘Mbagala’ na zingine zilizofuata, Diamond alitumia uhusiano wake na Wema kulibrand na kulipa nguvu zaidi jina lake. Alifanikiwa kwa hilo.

Fast forward kwa mara nyingine – mwaka 2014 – Diamond akaja kuwa msanii asiyehitaji tena kujitambulisha akiwa katika nchi yoyote Afrika kutokana na mafanikio aliyoyapata.

Kisha couple hiyo iliyokuwa na nguvu zaidi Afrika Mashariki ikaja kuvunjika.

Diamond akaangukia kwenye penzi la mwanamke tajiri, mrembo na mpenda skendo kama yeye mwenyewe, Zari aka The Bosslady wa Uganda. Wawili hao wanadaiwa kutarajia kupata mtoto.

Uhusiano wao ukawa gumzo si tu Tanzania, bali Afrika Mashariki nzima.

Lakini upande mwingine wa Wema mambo ni tofauti kidogo. Kwa muda sasa, Wema amekuwa hatengenezi tena headlines kama mwanzo ukilinganisha na kipindi kile yupo na Diamond. Habari kubwa na ya pekee iliyoandikwa hivi karibuni ni movie yake na muigizaji wa Ghana, Van Vicker.

Mbaya zaidi historia inaonesha kuwa Wema amefanikiwa kuwa na ushawishi huo kutokana na kuwa mtu wa kuandikwa sana kwenye magazeti ya udaku.

Sioni tena ile nguvu yake kama mwanzo. Hilo linanifanya nijiulize kuwa kuvunjika kwa uhusiano wao kumekuwa na madhara makubwa zaidi kwa Wema kuliko kwa Diamond? Wema ndiye aliyekuwa akihitaji zaidi uhusiano na Diamond ili ushawishi wake uendelee kuwa pale pale?

Nakubali kuwa Wema Sepetu ni brand inayojitegemea na kwa njia sahihi bado ataendelea kufanikiwa kisanaa, lakini ukweli unaonekana kuwa hazungumziwi sana kama zamani.

Wewe una mtazamo gani? Funguka hapo chini.

~Written By Fred Bundala