Mimi ni binti wa miaka 23, ninaishi na
wazazi wangu wote wawili, ni mtoto wa pili
kuzaliwa kwenye familia yetu. Nilianza
mahusiano ya kimapenzi nikiwa chuoni
mwaka wangu wa kwanza na kijana mmoja
aitwaye Erick, Nilitokea kumpenda sana
kwani alikuwa ndio mwanaume wangu wa
kwanza. Kwetu walimjua na hata kwao pia
nilifahamika.Nilikuwa na Erick mpaka
nilipofikamwaka wa pili hapo chuoni
Ambapo sasa tuliamua kukodi chumba
kimoja na kuishi wote. Katika kipindi hichi
niliona tabia za Erick hazieleweki anaweza
kurudi usiku sana akiwa hajitambui na hata
kulala tu chini mpaka asubuhi. Nilikuwa
nikimshauri lakini alikuwa ni mgumu sana
kunielewa.Siku moja alirudi akiwa mzima
majira ya saa kumi jioni hivi, kamasikosei
ilikuwa ni siku ya ijumaa, tena mimi nilikuwa
ndio natoka kwenye kipindi.Alikuja siku hiyo
akiwa na furaha sana huku akiwa na chupa
mbili moja ya wine na nyingine ya amarula,
Alizifungua zote nakuanza kunywa huku
tukipiga story na kucheka, na mimi
kwasababu pia nilikuwa nakunywa alini
miminia natukawatunakunywa wote, Nilipo
anza kulewa alianza kunishawishi nivute
sigara ambayo yeye alishaiwasha nakuanza
kuivuta bila kusita nilichukua sigara na
kuivuta kwakuwa nilimuamini sana
Erick.Muda si mrefu nilipata usingizi wa
ajabu ambao ulinifanya nisitambue
chochote kilichoendelea pale.Kesho yake
majira ya saa tano Asubuhi nilipata fahamu
na kuamka, nilimuuliza Erick kilichotokea
lakini hakunipa jibu lililo eleweka sikuwa na
raha kabisa kwani nilitamani kupata ileraha
tena, Nilishawishika kumuuliza erick kuhusu
myingine akasema vuta hii hapa.Huu ndio
ulikuwa mwanzo wa kuharibu masomo
yangu. Kumbe kipindi chote Erick alikuwa
anatumia madawa ya kulevya akichanganya
kwenye sigara, na akaona haitosha anipe na
mimi.Basi na mimi niliendelea na tabia hiyo
hadi darasani nikawa siendi tena walimu
walikuwa wananiulizia sana kwani nilikuwa
kati ya wanafunzi wazuri sana darasani.
Niliendelea na tabia hiyo hadi wazazi wangu
walipokuja kujua na kunipeleka kwenye
kituo cha waathirika wa madawa. Kipindi
hicho Erick alikuwa amechanganyikiwa
kabisa kwa madawa na chuo alisha acha
yuko tu kwao.Nilikaa huko kwenye kituo
hicho kwa muda wa miezi sita, nikiwa
napata ushauri pamoja na dawa za
kupunguza hamu ya madawa ya kulevya.
Nashukuru sasa hivi niko nyumbani na
ninaendelea vizuri.NAWASHAURI WANAVYUO
WAJARIBU SANA KUEPUKA VISHAWISHI
VINAVYOWEZA KUHARIBU MAISHA YAO KWA
UJUMLA!