Jana kwenye ibada ya mkesha wa kuupokea mwaka mpya uliooneshwa live star TV, Waziri Nyalandu alijitokeza wazi na kuongea kikampeni akiomba waumini wa dini ya Efata kumchagua kuwa Rais.
Isitoshe, Nyalandu aliongelea utawala wa Rais Kikwete kuwa ni utawala unaolindwa na majini saba, ingawa hakufafanua alimaanisha nini, lakini alishangiliwa sana na waumini wa Efata.
Anayejiita nabii na mtume Mwingira, naye aliongeza kuonesha wazi kuwa Nyalandu ndie chaguo lao.
My take: Huo ni udini wa wazi kabisa. Nyalandu ameanza kutumia kanisa analosali kuomba kura za waumini wake.
Kuna maneno ambayo yamemkosea adabu Mwenyekiti wa CCM, Professa Kikwete, kwamba analindwa na majini saba. Sina hakika kama maneno hayo ni rasmi ndani ya CCM au ni ya kanisa la Mwingira.
Wadau karibuni.