Nahodha huyo wa zamani wa England anamaliza mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na amechukua uamuzi mgumu wa kutoongeza mkataba mpya.
Liverpool walimpa ofa mpya Gerrard mwezi November mwaka jana lakini kiungo huyo mwenye miaka 34 alifikia uamuzi wa kutaka kwenda sehemu nyingine kupata changamoto mpya.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Liverpool Steven Gerrard ameelezea uamuzi wake wa kuondoka kwa kina:
‘Nimeamua kutangaza uamuzi huu sasa ili kocha na timu isipoteze umakiini kwenye mambo ya msingi kutokana na tetesi juu ya hatma yangu.
‘Liverpool Football Club ni sehemu kubwa ya maisha yangu na jambo hili la kuondoka hapa ni uamuzi mgumu zaidi niliowahi kufanya katika maisha yangu, lakini ni uamuzi ambao utakuwa na faida kwa watu wote wanaohusika, ikiwemo familia yangu na klabu yenyewe.
‘Nitaendelea kucheza soka lakini siwezi kuthibitisha wapi nitaenda baada ya kutoka hapa, ila kwa uhakika kabisa haitokuwa hapa nikimaanisha sitoichezea klabu ambayo itakuwa na upinzani au itacheza dhidi ya Liverpool – hilo ni jambo ambalo nawaahidi mashabikiwa Liverpool.” – Gerrard.
Geerard alianza rasmi kuitumikia Liverpool mnamo mwaka 1998, mpaka sasa anatajwa kuwa mmoja ya wachezaji bora kabisa wa muda wote wa klabu hiyo akiwa ameichezea mechi 695 , na kufunga magoli 177.
Haya hapa ni makombe ambayo amewahi kutwaa akiwa na Liverpool.
1 Champions League
2 FA Cups
3 League Cups
1 UEFA Cup
2 UEFA Super Cups
1 Charity Shield