Ni mara chache tumesikia viongozi wakubwa kwenye nafasi kama Rais akiomba radhi hadharani hata kama ni kweli amekosea.
Moja ya video zilizopata umaarufu mkubwa ndani ya saa chache ni hii inayoonyesha bibi na bwana wakiwa kwenye suti na shela, kwenye pilika pilika za sherehe ya ndoa kisha ikapigwa simu kutoka kwa Rais Obamaakiwaomba maharusi hao radhi kwa kuwahamisha sehemu ambayo ilikuwa sherehe ya wawili hao ifanyike.
Maafisa usalama wa Marekani walilazimika kuwahamisha maharusi hao katika eneo ambalo ilikuwa ifanyike sherehe yao kwa kuwa Rais Obamaalikuwa akienda kucheza gofu katika kipindi cha mapumziko.
Maharusi hao ambao wote ni wanajeshi, Kapteni Hiemel na KapteniMallue walipokea simu kutoka kwa Obama akiwaomba radhi kwamba alichelewa kupatiwa taarifa kuhusu shughuli ya maharusi hao kufanyika katika viwanja hivyo.
Hii ni video inayoonyesha maharusi hao wakiongea na Rais Obama.