Mambo vipi wakubwa? Inakuwaje wazazi hapo kwa fasi ya kitaa ya kati? Saidi hii ni mpango mzima. Unataka mambo matamtamu? Kaa humu wewe uwe mjanja. Mimi si ndo mjanja wenu? Basi barida. Ama nini?
Ebana mambo ya mapanya rodi sijui mapaka rodi hebu tuyapige dauni tusiwape kiki kiivo. Zaidi ya hapo tukimbizane na hili laifu hadi kieleweke chaliiangu.
Ebana wanangu kama mtu hukujipanga inabidi tukupange maana wewe utatumbuaje hadi umalize mshiko wote? Hivi mazee kachaa unashindwaje kujipanga? Kila kona vichwa vinamaindi huu mwezi dume…hivi mwanaume hukujua kuwa kuna mambo ya ada, makodi na mavitu mengine? Sasa mbona makachaa tunasebenza na kitu cha mizinga deile?
Sori makachaa nimeanza na makavu bati ni kwa sababu kuna mwanangu kanitibua kinoma aisee. Hebu imajini dizaini kama tuna majukumu kibwena dheni mtu anapiga mizinga! Halafu ukichomoa anakuona snichi. Huko si kutafutana ubaya wanangu?
Mwanangu Ino alitumbua kinoma wakati wa holidei za eksimasi na niu yia. Unaambiwa jamaa alikuwa anazungusha raundi kama hana akili nzuri. Watu weweee…kapachikwa jina la Pedeshee Kifaranga Mutoto ya Kuku. Unajua bana ukiwa vizuri utapewa masifa kibao hata kama siyo hendisamu utaambiwa ni hendisamu.
Kwa wachuchu ndo usiseme. Ilikuwa ni mwendo wa kubandika na kubandua. Mwanaume alikuwa fulu kero kitaa. Si unajua zile za kuwapotezea wana kisa una mkwanja mbuzi?
Kuna msela wangu alinitonya kwamba jamaa alikuwa kero kinoma alipotimba kileji kuhesabiwa kozi alijitoa fahamu eti anaosha ndinga na maji ya dhahabu! Yaani kweli maji ya mende watu wanayasikilizia mara moko kwa mwaka wewe unaoshea gari? Huo si ni umbulula wana?
Basi msela vichwa vimemvumilia kudadeki. Watu wanamminyia tu na kumcheki kama hawamuoni. Si unajua zile za kujifanya husikii kumbe unasikilizia tu wepesi na kujisemea kimoyomoyo walahi! Kafanya kufuru zake wee bati nawu yupo mweupeee…mbaya zaidi mwanangu si katumbua hadi msingi?
Samu taimu washikaji huwa wanajitoa fahamu na kuishi na ganzi bati kwa huyu mwanangu ilikuwa tuu machi. Wewe una akili gani unafagia hadi msingi? Hivi kichwani kunakuwa kumepotea skruu f’lani au kichwa kina michanga?
Ukimpiga chabo msela utamhurumia aisee maana hana ndururu na wale makiksi na vichenchede aliokuwa anamingo nao wamebonyea. Si unajua kama huna mawe kaka mkubwa mashori wote wakare utawaita shemu? Chezea kufulia ndani ya kitu cha mwezi dume?
Sasa bana mwanangu yupo anaungaunga kinoma. Yaani machizi nao wanajifanya hawamuoni maana alipokuwa na mawe alikuwa hawaoni. Homu nako fulu msala maana makidi wanatakiwa kwenda skonga na koleji na hapo bado faza hausi hajaanza kutaka chake. Utatamani ardhi ipasuke uzame bati ndo hivo tena atafanyaje zaidi ya kujikaza kiume?
Mazee wakati wa kutumbua ni beta ukajua kabisa kwamba unatafuna na masela au maduu wa sampo gani ili ukifulia waokoe jahazi lisizame arifu. Kama huamini ngoja situwesheni kama ya kachaa wangu ikupate. Hapo alipo anajuta kinoma na kukumbuka hizo gudi deizi!
Mmenisoma masela? Kama vipi ongeza spidi ya kusaka bingo. Sii yuu neksti wiki. Tchao!
Mmenisoma masela? Kama vipi ongeza spidi ya kusaka bingo. Sii yuu neksti wiki. Tchao!