Thursday, January 1, 2015

PAKA MZEE ZAIDI DUNIANI AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 24!


Paka aliyekuwa akitambulika rasmi kuwa ndio mzee zaidi duniani kwa sasa, amefariki dunia akiwa na miaka 24. 

Paka huyo aitwaye Poppy alizaliwa mwezi Februari mwaka 1990, mwezi ambao Nelson Mandela alitoka gerezani-, na alitambuliwa rasmi kama paka mkongwe zaidi duniani na rekodi za dunia za Guinness mwezi Mei mwaka huu. 
Alikuwa akiishi mjini Bournemouth, nchini Uingereza. 
Paka huishi kwa wastani miaka 15. 
Wataalam wanasema miaka miwili ya mwanzo baada ya kuzaliwa, kwa maisha ya paka ni kama miaka 25 ya binaadam. Baada ya hapo, kila miezi mitatu ya paka, ni kama mwaka mmoja wa binaadam. 
Kwa nadharia hiyo, Poppy alikuwa na miaka 114. 
Imeripotiwa pia kuwa paka mzee zaidi kuishi duniani alikuwa anaitwa Creampuff, aliyeishi Texas Marekani, ambaye alifika umri wa miaka 38.